Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh.Dkt Hussein Ali Mwinyi, aliyafungua mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA 2025) yaliyofanyika Visiwani Zanzibar kwenye uwanja wa Mao na kulipongeza Baraza kuafiki mashindano hayo kufanyikia Zanzibar kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye miundo mbinu ya michezo ikiwemo viwanja vya Mao, maisara na Amani complex
Aida wakati akiwahutubia washiriki na wananchi waliohudhuria kwenye ufunguzi huo alielezea umuhimu wa michezo kwenye afya kwa ujumla pia alitilia mkazo suala la kuilinda Amani kama kauli mbiu ya mashindano ilivyokuwa ikisema "Amani yetu ndio Amana yetu".
Mh.Dkt Hussein Ali Mwinyi kwenye ufunguzi wa mashindano ya BAMMATA yaliyofunguliwa tarehe 06 September 2025 Visiwani Zanzibar.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania Generali Jacob John Mkunda akiongea na washiriki pamoja na wananchi waliohudhuria ufunguzi wa michezo ya Majeshi Tanzania kwenye uwanja wa Mao visiwani Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh.Dkt Hussein Ali Mwinyi akifungua michezo ya BAMMATA 2025 visiwani Zanzibar kwenye uwanja wa Mao