Kanda ya Uhamiaji


Kanda ya Uhamiaji ni moja kati ya kanda nane zinazounda Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) ambacho ni chombo cha kitaalamu cha michezo kilichosajiliwa kihalali kwa lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za michezo kwa Vyombo vya Ulinzi, Usalama na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).Baraza hili lilianzishwa rasmi mwaka 1977.

Madhumuni ya BAMMATA ni kuendeleza mahusiano, urafiki na undugu baina ya Majeshi ya Ulinzi, Usalama na Idara Maalum za SMZ na wananchi kwa ujumla. Aidha, Baraza huendesha mashindano yake kwa kushirikisha michezo mbalimbali kila mwaka ambayo ni Mpira wa Miguu, Netiboli, Ngumi, Riadha, Mpira wa Mikono, Mpira wa Kikapu, Mieleka, Mpira wa Magongo, Shabaha na Kuogelea.