Kanda ya Zimamoto

Kanda ya Zimamoto

Kanda ya Zimamoto ni moja kati ya kanda nane zinazounda Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) ambacho ni chombo cha kitaalamu cha michezo kilichosajiliwa kihalali kwa lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za michezo kwa Vyombo vya Ulinzi, Usalama na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).Baraza hili lilianzishwa rasmi mwaka 1977.

Madhumuni ya BAMMATA ni kuendeleza mahusiano, urafiki na undugu baina ya Majeshi ya Ulinzi, Usalama na Idara Maalum za SMZ na wananchi kwa ujumla. Aidha, Baraza huendesha mashindano yake kwa kushirikisha michezo mbalimbali kila mwaka ambayo ni Mpira wa Miguu, Netiboli, Ngumi, Riadha, Mpira wa Mikono, Mpira wa Kikapu, Mieleka, Mpira wa Magongo, Shabaha na Kuogelea.

Habari na Matuikio katika Kanda ya Zimamoto

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Abbas akifungua mchezo wa mpira wa Pete Kati ya Timu toka kanda ya ZIMAMOTO na Timu toka Kanda ya MAGEREZA
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Abbas akifungua mchezo wa mpira wa Pete Kati ya Timu toka kanda ya ZIMAMOTO na Timu toka Kanda ya MAGEREZA
Soma zaidi 🡢