JWTZ NA POLISI WANG'ARA BUNGE MARATHON 2026 DODOMA

Dodoma, Aprili 18, 2026

Wanariadha kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) pamoja na Jeshi la Polisi Tanzania wameonesha kiwango cha juu cha ushindani katika mashindano ya Bunge Marathon 2026 yaliyofanyika leo na kuhitimishwa katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Kwa upande wa JWTZ kupitia timu ya Jeshi Stars, mwanariadha mahiri SGT Cecilia Ginonga aliibuka mshindi wa kwanza katika mbio za kilomita 21 kwa wanawake baada ya kuonesha uimara, kasi na ustahimilivu wa hali ya juu. Ushindi wake umeendelea kuthibitisha ubora wa wanariadha wa Jeshi katika mashindano ya kitaifa.

Katika mbio za kilomita 10 kwa wanawake, PTE Agness Protas naye aliendelea kung’ara kwa kushika nafasi ya pili, akionesha jitihada kubwa na kuipa heshima timu ya JWTZ katika mashindano hayo.

Kwa upande wa Jeshi la Polisi Tanzania, wanariadha wake pia walionesha ushindani mkubwa na kujipambanua vyema. Kwa wanaume CLP Josephat Joshuo Gisemo alifanikiwa kushika nafasi ya tatu katika mbio za kilomita 5, huku WP Hamida akishika nafasi ya tatu katika mbio za kilomita 21.

Aidha, WP Grace alishika nafasi ya tano katika mbio za kilomita 5, PC Ambrose akashika nafasi ya nne, na PC Kassim kumaliza katika nafasi ya sita kwenye mbio hizo hizo za kilomita 5.

Matokeo haya yanaakisi juhudi, nidhamu na maandalizi makubwa ya wanamichezo kutoka vyombo vya ulinzi na usalama, ambao wameendelea kuitangaza vyema Tanzania kupitia michezo.

Ushiriki na mafanikio yao katika Bunge Marathon 2026 ni ishara ya kuimarika kwa michezo ndani ya taasisi za serikali pamoja na mchango wao katika kukuza vipaji vya Michezo kitaifa.

Matukio katika picha

Wanariadha kutoka Jeshi la Wananchi JWTZ Pichani ni SGT Cecilia Ginonga na PTE Agnes Protas Bunge Marathon Dodoma

Wanariadha kutoka Jeshi la Wananchi JWTZ Pichani ni SGT Cecilia Ginonga na PTE Agnes Protas Bunge Marathon Dodoma

Timu ya wanariadha kutoka Jeshi la Polisi Tanzania (kutoka Kushoto) CPL Josephat Gisemo, WP Grace, PC Kalistus, Pc kassim na WP Hamida

Timu ya wanariadha kutoka Jeshi la Polisi Tanzania (kutoka Kushoto) CPL Josephat Gisemo, WP Grace, PC Kalistus, Pc kassim na WP Hamida

Pongezi kwa Mwanariadha SGT Cecilia Mshindi wa Kwanza KM 21

Pongezi kwa Mwanariadha SGT Cecilia Mshindi wa Kwanza KM 21