Katibu Mkuu Mstaafu wa BAMMATA Kanali Martin Msumari na Mwenyekiti Mstaafu Kanda ya Magereza ACP Maltilda Mlawaa wapokea Zawadi ya Tuzo

Mwenyekiti wa BAMMATA Brig Gen Said Hamis Saidi akiwakabidhi Tuzo Kanali Martin Msumari na ACP Maltilda Mlawa kwa kutumikia vyema Baraza katika nafasi zao kwa kipindi chote cha Zaidi ya Miaka minne kama Katibu Mkuu wa BAMMATA na Mwenyekiti wa Kanda ya Magereza, baada ya kupangiwa majukumu mengine na wakuu wa vymbo husika, tuzo hizo zilitolewa katika kikao cha kamati kuu ya BAMMATA Mkoani Lindi tarehe 07 Nov 2024.
Kanda ya Polisi yashiriki vikao vya EAPCCO GAMES
katika jiji la Addis Ababa Nchini Ethiopia kwa ajili ya kukagua miundombinu ya
michezo hiyo ambayo hujumisha nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,Burundi,Kenya,Rwanda,Sudan
na Uganda,kwa upande wa Tanzania iliwakilishwa na ACP Nkuba na A/Insp Saddy
Mrope,ambapo mashindano hayo yanakadiliwa kuanza kufanyika tarehe April 27 hadi
Mei 04 2025,Vikao hivyo vilianza Novemba 08 hadi 20, 2024.