KIKAO CHA MAANDALIZI BAMMATA

Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Wella amemuwakilisha Mkuu wa mkoa Paul Chacha katika ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Utendaji ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) kilichofanyika Tarehe 26 Machi 2026 katika ukumbi wa Hoteli ya JM Tabora.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho Wella ameishawishi kamati kuuchagua mkoa wa Tabora kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, akieleza kuwa mkoa huo una miundombinu ya kutosha ikiwemo viwanja vya michezo vinavyokidhi vigezo.

Mkuu huyo wa Wilaya amegusia suala la usawa wa kijinsia katika uongozi wa michezo, akibainisha kuwa bado kuna upungufu wa uwakilishi wa wanawake katika nafasi za juu za maamuzi.

Kikao hicho kililenga kujadili maandalizi na mikakati ya kufanikisha mashindano ya BAMMATA yanayotarajiwa kufanyika mwaka huu, huku mikoa ya Mwanza, Mbeya na Singida ikitajwa kuwa miongoni mwa maeneo yanayowania kuwa wenyeji wa mashindano hayo.

Matukio katika picha

Picha ya Pamoja ya Kamati Tendaji Pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh. Upendo Wella

Picha ya Pamoja ya Kamati Tendaji Pamoja na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mh. Upendo Wella

Mkuu wilaya ya Tabora Mh. Upendo Wella kwenye Ufunguzi wa kikao cha maandalizi ya Mashindano ya Bammata 2026

Mkuu wilaya ya Tabora Mh. Upendo Wella kwenye Ufunguzi wa kikao cha maandalizi ya Mashindano ya Bammata 2026

Brigedia Jenerali Saidi H. Saidi - Mwenyekiti BAMMATA

Brigedia Jenerali Saidi H. Saidi - Mwenyekiti BAMMATA

Naibu Kamishna (DCF) Kennedy C. Komba - Makamu Mwenyekiti BAMMATA.

Naibu Kamishna (DCF) Kennedy C. Komba - Makamu Mwenyekiti BAMMATA.

Luteni Kanali Said A. Shamuhuna - Katibu Msaidizi BAMMATA

Luteni Kanali Said A. Shamuhuna - Katibu Msaidizi BAMMATA