MEJA KASUI ACHAGULIWA RAIS WA KAMATI YA UFUNDI CISM

Pichani ni Meja Mohamed Haruna Kasui (JWTZ) akipongezwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Gen. Jacob John Mkunda (CDF), baada ya kutunukiwa hati katika Makao Makuu ya Jeshi.

Pongezi za dhati kwa mwana BAMMATA, Meja Mohamed Haruna Kasui, kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kamati ya Ufundi ya Mpira wa Kikapu (Basketball Sport Committee President - PCSC) katika Baraza la Michezo la Majeshi Duniani (CISM).

Atahudumu katika nafasi hiyo muhimu kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2026 hadi 2030, akiendelea kuiwakilisha vyema Tanzania, JWTZ na jumuiya ya michezo ya kijeshi duniani. Sambamba na jukumu hilo la kimataifa, Meja Kasui pia anahudumu kama Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF).

Mafanikio haya ni uthibitisho wa uwezo, weledi na uongozi bora unaojengwa kupitia BAMMATA, pamoja na mchango mkubwa wa JWTZ katika kukuza vipaji na viongozi wa michezo wenye ushindani katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

Hongera sana Meja Mohamed Haruna Kasui wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Dodoma, kwa mafanikio haya makubwa na kwa kuendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania na JWTZ katika jukwaa la kimataifa.

Matukio katika picha