Mwanariadha mahiri wa Tanzania kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Felix Simbu, anatarajiwa kushiriki katika mashindano makubwa ya kimataifa ya Boston Marathon yatakayofanyika Jumatatu, tarehe 20 Aprili 2026 nchini Marekani.
Akizungumza katika mahojiano na moja ya vyombo vya habari vya Marekani, Simbu ameweka wazi dhamira yake ya kufanya vizuri katika mbio hizo, akilenga kuendeleza heshima na mafanikio ya Tanzania katika medani ya riadha duniani.
Mwanariadha huyo anaamini maandalizi aliyofanya yatamwezesha kushindana kwa kiwango cha juu dhidi ya wakimbiaji bora kutoka mataifa mbalimbali.
Ushiriki wa Simbu katika Boston Marathon unaendelea kuonyesha mchango mkubwa wa wanajeshi wa JWTZ katika kukuza na kuendeleza michezo nchini, huku ukibeba matumaini ya kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa.
Mwanariadha mahiri wa Tanzania kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),SGT Felix Simbu