RAISI WA TBF AFANYA KIKAO CHA KWANZA MKOANI DODOMA

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (Tanzania Basketball Federation – TBF) limeanza rasmi ukurasa mpya wa maendeleo ya mchezo huo baada ya uongozi wake mpya kufanya kikao kazi cha kwanza na viongozi wa mikoa, kikao kilicholenga kuweka mikakati imara ya kukuza na kuongeza thamani ya mpira wa kikapu nchini.

Kikao hicho kiliongozwa na Rais wa TBF, Hasheem Thabeet, ambaye sasa anaongoza shirikisho hilo akiwa na dhamira ya kuleta mageuzi makubwa katika Mchezo wa basketball Tanzania. Thabeet, ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa ngazi ya kimataifa, ameweka wazi kuwa ushirikiano na mikoa ni msingi muhimu wa kufanikisha dira ya shirikisho.

Katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 19 Aprili 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Dodoma Hotel jijini Dodoma, viongozi wa mikoa walipewa maelekezo ya kusimamia na kutekeleza mipango na dira iliyowekwa na TBF kwa mwaka huu. Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa vipaji vinaibuliwa kuanzia ngazi ya chini na kuendelezwa hadi kufikia ushindani wa kitaifa na kimataifa.

Aidha, kikao hicho kimeweka msisitizo mkubwa katika kuimarisha ligi za mikoa, kuboresha miundombinu ya michezo, pamoja na kuongeza ushiriki wa vijana na wadau mbalimbali katika maendeleo ya mchezo huo. Uongozi mpya unaamini kuwa kwa kushirikiana kwa karibu na viongozi wa mikoa, Tanzania inaweza kuwa moja ya nchi kinara wa mpira wa kikapu barani Afrika.

Hatua hii ya TBF inaashiria mwanzo wa safari mpya yenye matumaini makubwa, ambapo kupitia uongozi wa Hasheem Thabeet na timu yake, wadau wa mpira wa kikapu wanatarajia kuona mabadiliko chanya yatakayoinua hadhi ya mchezo huo nchini.

Matukio katika picha

Pichani ni Raisi wa TBF Mh. Hasheem Thabeet Katikati na  Upande wa kushoto ni Makamu wa Raisi wa TBF Major Mohamed Kasui .

Pichani ni Raisi wa TBF Mh. Hasheem Thabeet Katikati na Upande wa kushoto ni Makamu wa Raisi wa TBF Major Mohamed Kasui .

Viongozi na wajumbe wakiendelea na mkutano uliofanyika Dodoma Hotel Mkoani Dodoma

Viongozi na wajumbe wakiendelea na mkutano uliofanyika Dodoma Hotel Mkoani Dodoma

Picha ya pamoja ya Viongozi wapya wa TBF pamoja na wajumbe waliohudhuria kikao

Picha ya pamoja ya Viongozi wapya wa TBF pamoja na wajumbe waliohudhuria kikao