TIMU ZA MAJESHI ZAFANYA VIZURI TUZO ZA BMT

Tunatoa pongezi za dhati kwa timu za majeshi kwa kuendelea kufanya vizuri na kuonyesha ushindani mkubwa katika sekta ya michezo nchini kupitia Tuzo za BMT zilizofanyika jijini Dar es Salaam. Mafanikio haya yanaendelea kudhihirisha mchango mkubwa wa vyombo vya ulinzi na usalama katika kukuza vipaji, nidhamu, uzalendo na maendeleo ya michezo Tanzania.

Katika hafla hiyo muhimu iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa michezo nchini, Meneja wa Timu ya Jeshi Stars Basketball na ABC, Meja Yahaya Mgaya, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Meja Mohamed Kasui, pamoja na Mwenyekiti wa JKT Queens, Meja Ryoba, walipata nafasi ya kushiriki na kuungana na viongozi wengine wa michezo katika kutambua na kuthamini mchango wa wanamichezo, viongozi na taasisi zilizofanya vizuri kwa mwaka huu.

Ushiriki wa viongozi hao unaonyesha namna taasisi za majeshi zinavyoendelea kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya michezo mbalimbali nchini, hususan mpira wa kikapu, kwa kuandaa timu zenye ushindani wa hali ya juu na kutoa fursa kwa vijana wenye vipaji.

Hongereni timu zote za majeshi kwa kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kupitia michezo. Mafanikio haya yawe chachu ya kuongeza juhudi, mshikamano na ari ya ushindi katika mashindano yajayo.

Matukio katika picha

Meneja wa Timu Jeshi stars basketball Na ABC, Meja Yahaya Mgaya, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Meja Mohamed Kasui, pamoja na Mwenyekiti wa JKT Queens, Meja Ryoba, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe Hizo.

Meneja wa Timu Jeshi stars basketball Na ABC, Meja Yahaya Mgaya, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Meja Mohamed Kasui, pamoja na Mwenyekiti wa JKT Queens, Meja Ryoba, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe Hizo.