Ushiriki wa Timu ya JWTZ Ya Mpira wa Kikapu katika Mashindano ya Majeshi Nchini Ujerumani
-kupitia-Jeshi-lake-waliandaa-shindano-tajwa-katika-Shule-ya-utimamu-wa-mwili-na-michezo-kijeshi-(Bundeswehr).jpg)
Timu ya Mpira wa kikapu ilishirikisha Kiongozi mmoja (Chief of delegation), Mwalimu na wachezaji idadi nane (08) walioshiriki mashindano ya kwanza ya Majeshi ya Dunia kwa Mpira wa kikapu (3 by 3) yaliyofanyika Warendorf nchini Ujerumani. Shindano hilo ni moja kati ya mashindano yanayoratibiwa na CISM ambapo Nchi mwenyeji (German) kupitia Jeshi lake waliandaa shindano tajwa katika Shule ya utimamu wa mwili na michezo kijeshi (Bundeswehr). Jumla ya Mataifa 16 ikiwa ni jumla ya timu 23 za Wanaume na Timu kumi (10) za wanawake zilishiriki.Licha ya changamoto na itifaki za ugonjwa wa Uvico 19 duniani, idadi ya washiriki ilikua ni zaidi ya 250 na watazamani (Spectactors) waliokadiriwa ni kufikia 200,000.
Mwaliko wa Ushiriki
Kurugenzi ilipokea mwaliko rasmi wa mashindano mnamo tarehe 19 May 22, ambapo taratibu za awali za maandalizi zilifanyika.Kibali cha kushiriki kilitolewa mnamo tarehe 15 Jun 22 na hivyo maandalizi stahiki ikiwepo kuanza Kambi yaliendelea.
Kuagwa na Kukabidhiwa Bendera
Timu iliagwa rasmi katika ukumbi wa TAU tarehe 01 Jul 22 na kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Brig Comd 302 KV Brig Gen SB Gwaya. Aidha timu hiyo iliagwa pia tarehe 02 Jul 22 na Viongozi wa Chama cha Basketball Tanzania na wadau baadhi wa Basketball nchini kwa kuwatakia kheri na fanaka katika mashindano.
Ufunguzi wa Mashindano rasmi
Mashindano yalifunguliwa rasmi mnamo TNS 041800c Jul 22 katika eneo maarufu la soko la Warendolf. Aidha mgeni rasmi kwa upande wa CISM alikua ni Makamu wa Raisi wa CISM Maj Gen Abdullah Maikano wakati kwa upande wa Ujerumani alikuepo Meya wa Mji wa Warendolf Mrs D. Kaiser na Brig Gen D. Mayerhoff (The Regional Comd-North Rhine Westphalia). Mamia ya wadau mbalimbali walishuhudia.
Ufunguzi wa Mashindano rasmi
Mashindano yalifunguliwa rasmi mnamo TNS 041800c Jul 22 katika eneo maarufu la soko la Warendolf. Aidha mgeni rasmi kwa upande wa CISM alikua ni Makamu wa Raisi wa CISM Maj Gen Abdullah Maikano wakati kwa upande wa Ujerumani alikuepo Meya wa Mji wa Warendolf Mrs D. Kaiser na Brig Gen D. Mayerhoff (The Regional Comd-North Rhine Westphalia). Mamia ya wadau mbalimbali walishuhudia.
Mashindano na Matokeo
1. Wanaume
Kwa upande wa wanaume timu
inekuwa miongoni mwa timu tano (05) bora ambapo imepata fursa ya kushiriki
mashindano ya Majeshi ya Dunia yajayo nchini Lithuania kama ifuatavyo:-
(a) Mshindi wa kwanza – Lithuania.
(b) Mshindi wa pili – France.
(c) Mshindi wa tatu – USA.
(d) Mshindi
wa Nne – Tanzania.
(e) Mshindi wa Tano – Morocco.
Aidha,
timu ya JWTZ ilifuzu hatua za awali za makundi, kabla ya kucheza katika kundi
la 16 bora (Sweet Sixteen). Wachezaji walijawa hamasa na saikolojia nzuri
ambapo kwa jitihada, uzalendo wa kweli, na kujituma ilifanikiwa kuingia robo
fainali baada ya kumfunga Mwenyeji nchi ya Ujerumani (Team 1 & 2) na
Morocco hatimaye kutinga hatua ya Nusu fainali.
Hata
hivyo timu ya JWTZ ilipoteza mchezo dhidi ya Ufaransa na USA na kushika nafasi ya nne (04) nyuma ya
USA.
2.
Wanawake
Timu
ya Wanawake walianza mashindano kwa mtindo wa ligi ambapo kila timu ilicheza na
nyingine. Michezo mitatu au zaidi ilichezwa kwa siku kwa kila timu. Licha ya
kuonyesha mchezo wa ushindani na uungawana muda wote kwa kadri mashindano
yalivyoendelea, timu ya JWTZ ilishindwa kwa kutolewa katika robo fainali ya
kwanza kwa mchezo dhidi ya Uholanzi.
Mafanikio
(Tuzo) zilizopokelewa
Timu
ya JWTZ (Tanzania) ilipeperusha bendera vyema kwa mafanikio ifuatavyo:-
(1) Kukabidhiwa tuzo maalumu ya Timu bora kutoka
CISM.
(2) Kamati ya Ufundi na Maandalizi ya mashindano
(CISM Basketball Technical and Organizing Committee), iliiteua timu ya wanaume ya JWTZ kuwa timu bora ya
mashindano.
(3) Timu ya JWTZ kupewa Kikombe cha Nidhamu na
mchezo wa kiungwana (CISM Fair
Play Trophy).
(4) Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano, MT 121613 Cpl Baraka Sadick Athumani (The most Variable player of 3 on 3 challenge)
ambaye pia alionyesha umahiri kwenye shindano la mitupo huru ya alama tatu (3
points competition) kwa kufikia hatua ya nusu fainali.
(5) Kamati ya ufundi ya CISM kwa mchezo huo kuwateuwa
P 10602 Capt MH Kasui (SO PT&S)
na Ssgt Haleluya Kavalambi (Coach)
kuunda kamati ya ufundi ya CISM kwa mchezo wa Basketball.
(6) Uwezekano wa kupata fursa za Wanajeshi wetu
wanamichezo kucheza Kimataifa (Professional athletes) badala ya kujitolea
(amateur) ambapo nchi za S. Arabia, Bangladesh
na Morocco yameonyesha nia kuwasajili wachezaji wa JWTZ kwa mkataba wa
malipo.
Sherehe
za Ufungaji
Sherehe ya ufungaji wa
Mashindano zilifanyika kwa Gwaride rasmi na Brass Band katika eneo la chuo cha
utimamu wa mwili na michezo – Bundeswehr. Meya wa jiji na Rais wa Baraza la Michezo
ya Majeshi la Africa (OSMA) Maj Gen A. Maikano walifunga rasmi shughuli za
michezo kwa hotuba fupi na kukabidhi bendera rasmi kwa nchi mwenyeji kwa mwaka 2023 Taifa la Luthiania.