KUHUSU SISI

Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) ni chombo cha kitaalamu cha michezo kilichosajiliwa kihalali kwa lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za michezo kwa Vyombo vya Ulinzi, Usalama na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).Baraza hili lilianzishwa rasmi mwaka 1977, Likijumuisha kanda  nane ambazo ni Kanda ya Ngome, kanda ya JKT, Kanda ya Polisi, Kanda ya Magereza, Kanda ya Uhamiaji, Kanda ya Zimamoto, Kanda ya Visiwani na Kanda ya SMZUTAN...
Soma zaidi 🡢

Habari na Matukio

TIMU ZA MAJESHI ZAFANYA VIZURI TUZO ZA BMT

TIMU ZA MAJESHI ZAFANYA VIZURI TUZO ZA BMT

Tunatoa pongezi za dhati kwa timu za majeshi kwa kuendelea kufanya vizuri na kuonyesha ushindani mkubwa katika sekta ya michezo nchini kupitia Tuzo za BMT zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA 81 CISM NCHINI MONACO

TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA 81 CISM NCHINI MONACO

Mkutano Mkuu na Kongamano la 81 la Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani International Military Sports Council umeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha majeshi duniani kupitia michezo, huku hafla rasmi ya ufunguzi iliyofanyika tarehe 4 na 5 Mei 2026 katika Principality of Monaco ikiweka...
TIMU YA TAIFA YA MCHEZO WA PETE KUPEPERUSHA BENDERA YA ZANZIBAR NCHINI KENYA

TIMU YA TAIFA YA MCHEZO WA PETE KUPEPERUSHA BENDERA YA ZANZIBAR NCHINI KENYA

Timu ya mchezo wa Pete (Netball) inatarajia kushiriki mashindano ya klabu Bingwa Africa yatakayofanyika nchini Kenya. Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, yakizikutanisha klabu bora kutoka ukanda huu, huku yakiwa ni fursa muhimu kwa wachezaji wetu kuonesha vipaji vyao na kupata uzoefu wa...
RAISI WA TBF AFANYA KIKAO CHA KWANZA MKOANI DODOMA

RAISI WA TBF AFANYA KIKAO CHA KWANZA MKOANI DODOMA

Shirikisho la Mchezo wa kikapu Tanzania TANZANIA BASKETBALL FEDERATION (TBF) limefanya kikao cha Kwanza mwaka huu 2026 baada ya uchaguzi uliofanyika mwanzoni mwaka huu kuchagua viongozi wapya. Kikao hicho kiliongozwa na Rais wa TBF, Hasheem Thabeet, ambaye sasa anaongoza shirikisho hilo akiwa na dhamira...
JWTZ YANG’ARA KWA KISHINDO TANFOAM MARATHON 2026 ARUSHA

JWTZ YANG’ARA KWA KISHINDO TANFOAM MARATHON 2026 ARUSHA

Mashindano ya TANFOAM Marathon yaliyofanyika leo tarehe 19 Aprili 2026 jijini Arusha yameacha alama kubwa katika ulimwengu wa riadha nchini, huku wanariadha wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakionesha ubora wa hali ya juu, nidhamu na ushindani wa kimataifa katika mbio za kilomita...
MWANARIADHA SSGT FELIX SIMBU KUIWAKILISHA TANZANIA BOSTON MARATHON 2026 NCHINI  MAREKANI

MWANARIADHA SSGT FELIX SIMBU KUIWAKILISHA TANZANIA BOSTON MARATHON 2026 NCHINI MAREKANI

Mwanariadha mahiri wa Tanzania kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Felix Simbu, anatarajiwa kushiriki katika mashindano makubwa ya kimataifa ya Boston Marathon yatakayofanyika Jumatatu, tarehe 20 Aprili 2026 nchini Marekani
JWTZ NA POLISI WANG'ARA BUNGE MARATHON 2026 DODOMA

JWTZ NA POLISI WANG'ARA BUNGE MARATHON 2026 DODOMA

Wanariadha kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) pamoja na Jeshi la Polisi Tanzania wameonesha kiwango cha juu cha ushindani katika mashindano ya Bunge Marathon 2026 yaliyofanyika leo na kuhitimishwa katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.
TANZANIA YANG'AA RIADHA KIMATAIFA

TANZANIA YANG'AA RIADHA KIMATAIFA

Tanzania imeendelea kung'ara katika anga la michezo ya kimataifa baada ya timu ya riadha ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kufanya vizuri kwenye mashindano ya Majeshi ya Dunia.