Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) pamoja na Jeshi la Polisi zashiriki " 2nd Military All African Games"

Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lashiriki mashindano ya " 2nd Military All African Games" yanayofanyika katika jiji kuu la Abuja Nchini Nigeria,katika mashindano hayo JWTZ kushiriki jumla ya michezo mitatu ambayo ni GOLF, BOXING & MARATHON, mashindano hayo yalianza tarehe 18 – 30th Nov 2024.
USHINDI KATIKA MARATHON
Alphonce Simbu amefanikiwa
kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania kwa upande wa (JWTZ NGOME) kwa kushika nafasi
ya Kwanza kupata MEDAL ya GOLD katika Mbio za KM 42 Marathon ya 2nd
Military All African Games iliyofanyika Abuja Nigeria
Magdalena Shauri
amefanikiwa kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania kwa upande wa
Wanawake (JWTZ NGOME) kwa kushika nafasi ya Kwanza kupata MEDAL ya
GOLD katika Mbio za KM 42 Marathon ya 2nd Military All
African Games iliyofanyika Abuja Nigeria
Transfora Mussa wa Kanda ya POLISI TANZANIA ameshika
nafasi ya Kwanza upande wa Wanawake na kujinyakulia Medali ya GOLD
katika Mbio za Fulham KM 10 Uingereza
Alitumia dk 31:53 akivunja rekodi ya mshindi wa 2023 kutoka
Kenya aliekimbia kwa muda wa dk 33;11 katika mshindano hayo ya Fulham
Uingereza.
Bondia wa JWTZ Yusuf Changalawe kushinda pambano kwa KO baada
ya kumpiga Mnaigeria katika mashindano ya 2nd Military All
African Games yaliyofanyika Abuja nchini Nigeria tarehe 19 Nov 2024.