JWTZ yashiriki michezo ya majeshi -Nairobi Kenya 2019

JWTZ lilishiriki katika Mzunguko wa 12 wa Michezo ya Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki “EAC” iliyofanyikia Nairobi, nchini Kenya kuanzia tarehe 11 – 24 Aug 19. Pamoja na Tanzania washiriki wengine ni kutoka Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini na Uganda. Michezo iliyoshirikishwa ni Mpira wa Miguu wanaume, Mpira wa Netiboli wanawake, Mpira wa Wavu wanawake, Mpira wa Kikapu wanaume na Mbio za Nyika kwa wanaume na wanawake.

SHEREHE ZA UFUNGUZI, UFUNGAJI NA HAFLA YA UFUNGAJI
Sherehe za ufunguzi zilifanyika tarehe 13 Aug 19 katika uwanja wa Kasarani ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri wa Ulinzi wa Kenya, Mh. Balozi Raychelle Omamo. Aidha, Sherehe za ufungaji zilifanyika tarehe 23 Aug 19 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Kenya, Mh. Rais Uhuru Kenyatta. Aidha, sherehe hizo za ufungaji zilihudhuriwa na wafuatao :-
 a.      Burundi - Mhe: Emanuel Ntahomvukya – Waziri wa Ulinzi
 b.      Kenya - Mhe Reychelle Omamo (SC) – Waziri wa Ulinzi na Gen Samson Mwathethe – Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.
 c.      Rwanda - Gen  Patrick Nyanvumba – Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.
 d.      Sudan Kusini - Mhe: Eng Kuol Manyang Jak – Waziri wa Ulinzi. na Lt Gen Gabriel Jok Riak – Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.
 e.      Tanzania - Maj Gen SS Othman – GOC DFHQ COMD
  f.      Uganda - Gen David R. Muhoozi – Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.
 
MATOKEO KWA TIMU ZETU
Matokeo kwa timu zetu yalikuwa ifuatavyo:-
a. Mpira wa Miguu Wanaume:-
        (1) Tanzania 7:3 Burundi
        (2) Tanzania 2:1 Kenya
        (3) Tanzania 1:3 Rwanda
        (4) Tanzania 0:2 Uganda
 
b. Mpira wa Pete Wanawake:-
        (1) Tanzania 99:16 Burundi
        (2) Tanzania 40:46 Kenya
        (3) Tanzania 66:16 Rwanda
        (4) Tanzania 34:49 Uganda
 
c. Mpira wa Kikapu Wanaume:-
        (1) Tanzania 75:79 Burundi
        (2) Tanzania 78:85 Kenya
        (3) Tanzania 54:83 Rwanda
        (4) Tanzania 55:78 Uganda
         (5) Tanzania 62:93 Sudani Kusini
 
d. Mpira wa Wavu Wanawake:-
        (1) Tanzania 3:1 Burundi
        (2) Tanzania 2:3 Kenya
        (3) Tanzania 0:3 Rwanda
         (4) Tanzania 0:3 Uganda
 
e. Riadha Wanaume:-
        (1) Kenya
        (2) Tanzania
         (3) Uganda
         (4) Rwanda
         (5) Burundi
         (6) Sudani Kusini
 
f. Riadha Wanawake:-
        (1) Kenya
        (2) Uganda
        (3) Tanzania
        (4) Rwanda
        (5) Burundi
 
TUZO BINAFSI ZA WACHEZAJI BORA
Pamoja na matokeo ya ujumla kutokuwa ya kuridhisha, Tanzania iliongoza kwa kunyakua tuzo za mchezaji mmoja mmoja (vipaji binafsi) kutokana na uwezo na vipaji walivyoonesha katika michezo ya Majeshi ya EAC 2019 kama ifuatayo:-
a.     Cpl Mwanaidi Hassan Ngubege – Mfungaji bora – Mchezo wa Netiboli.
b.     Cpl Fully Zulu Maganga – Mfungaji bora – Mpira wa Miguu
c.     Pte Joyce Edward Kaila – Mlinzi bora – Mchezo wa Netiboli
d.     Pte Baraka Sadick Athumani – Mfungaji bora – Mchezo Mpira wa Kikapu
e.     Pte Magdalena Crispin Shauri – Mshindi wa kwanza wa Riadha kwa Wanawake (Medali ya Dhahabu)