Mashindano ya Majeshi (CISM) Wuhan China 2019

JWTZ yashiriki michezo ya
CISM ikijumuisha michezo ya mieleka,
riadha na ngumi Wuhan China mwaka 2020.
1. Timu Teule ya Mchezo wa
Ngumi “Boxing”
Timu Teule ya Mchezo wa Ngumi
ilishiriki Michezo ya Majeshi ya Dunia (CISM) iliyofanyika mjini Wuhan nchini
China kuanzia tarehe 18 Oct 19 hadi tarehe 27 Oct 19 na matokeo yalikuwa
ifuatavyo:-
Tarehe 18/10/19 timu ya ngumi
ilianza kushiriki michezo hiyo kwa meneja na kocha kushiriki katika kikao
(technical meeting) kupata maelekezo ya mashindano na kufanya “draw”. Michezo
ilichezwa kwa mtoano.
a. Tarehe
19/10/19 mabondia wanne (4) wa Tanzania walipanda ulingoni kupeperusha bendera
ya Tanzania kulingana na matokeo ya “draw’
b. Matokeo
ya jumla Cpl Seleman Kidunda ameshika nafasi ya tano (5) katika uzito wa 75 Kg
na kutunukiwa cheti cha ushindi.
c. Sgt
Burhani Abdallah alicheza dhidi ya Poppe (German). Matokeo Sgt Burhani
alishindwa kwa Tush (KO).
d. Cpl
subiri Mwanzembe aliyecheza uzito wa 57 Kg (Free Style) peke yake alipata cheti
cha ushindi wa nafasi ya tano.
e. Sgt
Burhani Abdallah alicheza dhidi ya Poppe (German). Matokeo Sgt Burhani
alishindwa kwa Tush (KO).
f. Cpl
subiri Mwanzembe aliyecheza uzito wa 57 Kg (Free Style) peke yake alipata cheti
cha ushindi wa nafasi ya tano.
2. Timu Teule ya Riadha
Timu Teule ya Riadha ilishiriki
Michezo ya Majeshi ya Dunia (CISM) iliyofanyika mjini Wuhan nchini China kuanzia
tarehe 18 Oct 19 hadi tarehe 27 Oct 19 na matokeo yalikuwa ifuatavyo:-
a. Track
and Field: Katika sehemu hii ya mchezo wa Riadha, mashindano yalifanyika
kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa mara baada ya kamati ya ufundi kuridhia.
(1) Umabali
1500m: Tarehe 26 Oct 19, Mshiriki wetu Pte Cesilia Panga alishiriki mbio za
fainali za 1500m (wanawake) na kushika nafasi ya 10 kati ya washiriki 21.
(2) Umbali
10,000M: Tarehe 23 oct 19 saa 19:20 mbio za mita 10000 zilichezwa kama fainali
bila kupita makundi (Elimination stage) JWTZ lilikua na washiriki wawili
na matokeo yao ni kama ifuatavyo:-
(a) Pte
Gisamoda Giniki – Alishika nafasi ya nne kati ya washiriki 36 toka nchi
mbalimbali.
(b) SM Sylnester Marko – Alishika nafasi ya sita kati ya washiriki 36.
(3) Umbali
5000M: Tarehe 24 Oct 19 saa 0930 washiriki wetu wawili walicheza hatua ya awali
5000m na kufanikiwa kupita hatua ya fainali. Hatua ya awali ilikuwa na jumla ya
washiriki 40. Wachezaji wetu wawili wafuatao waliofaulu kuingia hatua na
fainali ya wachezaji 15:-
(a) Pte
Faraja Damasi
(b) Pte
Panga Joseph.
Pte Faraja Damasi – alishika nafasi ya sita (6) katika mbio za mita 5,000 na Pte Panga Joseph – alishika nafasi ya nane (8) katika mbio za mita 5,000.
(4) Marathon
(42.195 Km): Mchezo wa pili kwa upande wa riadha ilihusisha mbio ndefu Full
Marathon 42.195km mnamo TNS 270800C 0ct 19. Katika mchezo huo (Men’s individual
Marathon):-
(a) Pte
Alphonce Simbu alipata nafasi ya pili (2) kati ya washiriki 97 waliokuwa kwenye
orodha na washiriki 87 waliomaliza mbio hizo.
(b) Mshiriki
wa pili kwa upande wa marathon Cpl Ezekiel Ng’imba hakuweza kumaliza mbio
kutokana na majeraha ya kisigino.
(c) Mbio hizi Cpl Alphonce Simbu alipata
Medali ya Fedha (Silver Medal) kwa kukimbia kwa muda wa 2:11:16, Mkuu wa
Majeshi kwa niaba ya Jeshi alimpongeza kwa kupata matokeo hayo mazuri na
kupandishwa cheo toka PTE na kuwa CPL. Pamoja na kupata medali ya Fedha
(Silver) kupitia kwa Cpl Alphonce Simbu,
wachezaji wengine watano wa
riadha walitunukiwa vyeti vya ushindi ifuatavyo:-
a. Pte Gisamoda Giniki alishika nafasi ya nne (4) katika mbio za
mita 1000
b. Servieman Sylivester Marko alishika nafasi
ya sita (6) katika mbio za mita 1000
c. Pte
Faraja Damasi alishika nafasi ya sita (6) katika mbio za
mita 5000
d. Pte Panga Joseph alishika nafasi ya nane (8)
katika mbio za mita 5000
e. Cpl Magdalena Shauri alishika nafasi ya nane
katika mbio za mita 5000